×

注意!页面内容来自https://www.msdmanuals.com/sw/home/quick-facts-infections/covid-19/covid-19,本站不储存任何内容,为了更好的阅读体验进行在线解析,若有广告出现,请及时反馈。若您觉得侵犯了您的利益,请通知我们进行删除,然后访问 原网页

COVID-19

(Ugonjwa wa kirusi cha Korona 2019; COVID)

Imepitiwa/Imerekebishwa Imebadilishwa Oct 2025
v58273872_sw

JeCOVID-19 ni nini?

COVID-19 ni maambukizi hatari ya virusi ambayo huathiri zaidi mapafu na njia zako za hewa.

  • Husababishwa na kirusi cha korona

  • Virusi husambaa kwa urahisi kwa watu wengine

  • Baadhi ya watu walioambukizwa hawana dalili au wana dalili ndogolakini wengine huugua sanana baadhi ya watu hufa

  • Pamba zilizotumika kupangusa pua na koo lako hupimwa ili kutambua uwepo wa COVID-19

  • Hakuna dawa ya kuponya COVID-19lakini baadhi zinaweza kusaidia watu walio na maambukizi makali au watu walio katika hatari ya kupata maambukizi makali

  • Njia bora zaidi ya kuzuia COVID-19 ni kupata chanjo

Jenini husababisha COVID-19?

COVID-19 husababishwa na aina ya kirusi cha korona kinachoitwa SARS-CoV-2. Virusi huenea:

  • Hasa kupitia hewakwenye matone ambayo mtu mwenye maambukizi husambaza kupitia kukohoakupiga chafyakuimba au kuzungumza

  • Kupitia kugusa vitu ambavyo mtu mwenye maambukizi amevigusa na kisha kugusa uso wake

Unaweza kusambaza kirusi kinachosababisha COVID-19 hata kabla ya kupata dalili yoyote.

PiaCOVID-19 husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa urahisi zaidi kuliko maambukizi mengine ya njia za upumuaji kama vile mafua au homa ya mafua

Jekirusi cha korona ni nini?

Kuna mamia ya virusi mbalimbali vya korona ambavyo vyote vinahusiana. Vingi kati ya virusi hivi huambukiza wanyama tu.

  • Ni virusi vichache tu vya korona vinavyoweza kuambukiza watu

  • Baadhi husababisha mafua

  • Virusi vitatu vya korona husababisha ugonjwa mkali na vinaweza kusababisha umauti

Mbali na COVID-19maambukizi mengine makali ya virusi vya korona huitwa SARS na MERS. Ni vigumu mtu yeyote kupata maambukizi hayo tena.

Jedalili za COVID-19 ni zipi?

Watu wengi wenye COVID-19 huwa hawana dalili hata moja.

Ikiwa utapata dalilikuna uwezekano mkubwa utakuwa na:

  • Homa

  • Kikohozi kikavu

  • Kupumua kwa shida

  • Kuhisi udhaifu na uchovu mwingi

Huenda pia:

  • Pua zinazotoa kamasi

  • Maumivu kooni

  • Kupoteza hisia ya kunusa na ladha

  • Maumivu ya kichwa

  • Matatizo ya tumbo kama vile kichefuchefukutapika na kuhara

Maambukizi makali huingia kwenye mapafu yakona kusababisha nimonia inayosababishwa na virusi. Hali hii itakufanya ushindwe kuvuta pumzi ya kutosha Maambukizi makali yanaweza kuathiri ogani nyingipamoja na ubongomoyo na figo.

JeCOVID-19 inaweza kusababisha umauti?

Unaweza kufa kutokana na COVID-19. Jinsi ambavyo una umri mkubwandivyo hatari yako ya kifo inavyoongezeka. Vifo vingi hutokea kwa watu wenye umri unaozidi miaka 50. Watu wenye umri unaozidi miaka 80 wako kwenye hatari kubwa sana. Lakini watoto na vijana wanaweza kufa.

Pia uko kwenye hatari zaidi iwapo una matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa moyounene kupita kiasiau kisukari.

Jeninawezaje kufahamu kuwa nina COVID-19?

Unapaswa kufanya kipimo cha COVID-19 iwapo:

  • Una dalili za COVID-19—unapaswa kujitenga wakati ukisubiri matokeo ya vipimo

  • Ulikuwa karibu na mtu mwenye COVID-19 (wewe ni "mtu wa karibu")

  • Uliombwa kupima kazinishuleniau upimaji wa jumuiyahasa ikiwa hujapokea chanjo kamili

Kipimo maarufu ambacho daktari au mfanyakazi wa huduma za afya atakufanyiakinaitwa kipimo cha PCR (kipimo cha mwitikio wa mnyororo wa polima)na hutumia:

  • Pamba zilizotumika kupangusa pua au koo lako

Pamba hizo hutumwa kwenye maabara ili kutafuta kirusi au ushahidi mwingine wa maambukizi. Inaweza kuchukua siku kadhaa hadi upate matokeo yako.

Vipimo vya antijeni ni aina tofauti ya kipimo ukilinganisha na kipimo cha PCR. Vipimo vya antijeni vinaweza kufanyika nyumbani au kwenye mazingira ya huduma za afya na hutumia pamba iliyotumika kupangusa ndani ya pua yako. Kwa ujumla havina ufanisi ukilinganisha na vipimo vya CPR. Lakini vipimo vya antijeni vinaweza kutoa matokeo ya haraka (ndani ya dakika 15)

Kipimo cha damu kinaweza kutafuta uwepo wa kingamwili ambayo mwili wako umeitengeneza kupambana na kirusi. Huchukua mwili wako wiki chache kuunda kingamwilihivyo kipimo hiki hakina manufaa pale unapoumwa kwa mara ya kwanza. Lakini kinaweza kukusaidia kujua kama umewahi kupata maambukizi.

JeCOVID-19 inatibiwa vipi?

Iwapo una hali kiasi au wastaniunaweza:

  • Kukaa nyumbani na kutotoka nje au kusogelea watu wengine (kujitenga)

  • Kuvaa barakoa ili usisambaze virusi

  • Kutumia acetaminophen au ibuprofeni kwa ajili ya homa na maumivu

Ikiwa una hali mbaya kwa matatizo ya kupumuautapaswa kwenda hospitali. Madaktari watafanya:

  • Kukupa oksijeni

  • Wakati mwinginewatakupatia dawa

  • Wakati mwinginekukuweka kwenye kipumuaji (mashine ya kukusaidia kupumua)

Unaweza kutakiwa kukaa kwenye kipumuaji kwa wiki kadhaa.

Ikiwa figo zako zina matatizounaweza kuhitaji huduma ya kusafisha damu.

Jeninawezaje kuzuia COVID-19?

Njia bora zaidi ya kuzuia COVID-19 ni kupata chanjo. Mwongozo kuhusu chanjo ya COVID-19 umebadilika baada ya muda. Angalia mapendekezo ya Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC)Chuo cha Madaktari wa Watoto cha Marekani (AAP)na Chuo cha Madaktari wa Familia cha Marekani (AAFP) kwa maelezo zaidi.

  • Chanjo ni salama na zenye ufanisi

  • Huwezi kupata COVID-19 kutoka kwenye chanjo ya COVID-19

  • Ufanisi wa chanjo unaweza kupungua kadiri muda unavyokwendahivyo ni muhimu kuchoma chanjo ya hivi karibuni

  • Chanjo za COVID-19 zinaweza kuwa na athari za kando kiasi (kidonda kwenye mkonomaumivu ya mwilimaumivu ya kichwahoma) kwa siku moja au mbili

  • Unapaswa kupata chanjo ya COVID-19 hata kama ulipata maambukizi ya COVID-19

Zaidi ya kupata chanjounapaswa kuepuka kukaribiana na virusi. Hilo linaweza kuwa jambo gumu. Watu wanaoweza kueneza virusi wanaweza wasiwe na dalili zozotekwa hivyo huwezi kujua ni nani aliye navyo na nani hana. CDC inapendekeza njia za ziada za kusaidia kuepuka virusi katika Kuzuia Ugonjwa wa Upumuaji wa CDC.

Unapaswa kuvaa barakoa inayokuenea vizuri usoniikifunika mdomo na pua:

  • Wewe au watu walio karibu nawe mna sababu za hatarishi ya ugonjwa mbaya.

  • Wewe au watu walio karibu nawe mliambukizwa virusi vya upumuaji hivi karibunini wagonjwaau mnapata nafuu.

  • Virusi vya upumuaji vinasababisha magonjwa mengi katika jumuiya yako.

Zingatia kuvaa barakoa unapokuwa kwenye usafiri wa umma (kwa mfanondegebasitreni) na wakati ukiwa ndani ya vituo vya kusubiri usafiri (kwa mfanouwanja wa ndegekituo cha treni).

Mbali na kuwa umechoma chanjo za hivi karibuni na kuvaa barakoa:

  • Kupima ikiwa una dalili za COVID-19

  • Kujiepusha na maeneo yenye watu wengi na maeneo ya ndani ambayo ya upungufu wa hewa safi inayotoka njeiwapo uko kwenye hatari ya kuumwa sana kutokana na COVID-19

  • Dumisha umbali unaofaa wa kijamii kutoka kwa watu wengine ikiwa huna chanjo kamilihasa ikiwa uko katika hatari kubwa ya kuugua sana kutokana na COVID-19

  • Dumisha umbali mzuri wa kijamii kutoka kwa mtu aliye mgonjwa wa COVID-19 

  • Osha mikono yako kila mara kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20

  • Tumia kitakasa mikono chenye pombe

  • Epuka kugusa machopua na mdomo kwa mikono ambayo haijaoshwa

  • Baki nyumbani pale unapoumwa

  • Funika mdomo kwa karatasi ya shashi pale unapokohoa au kupiga chafyakisha itupe kwenye taka

  • Safisha na takasa kila mara vitu na sehemu za juu zilizogushwa kwa kutumia kinyunyizio au kifuto cha kawaida cha nyumbani

  • Zingatia afya yako na fuatilia dalili zako

Karantini na Kutengwa

Hatua za karantini na kutengwa zimependekezwa katika jaribio la kupunguza kuenea kwa mlipuko huu wa ndanikikanda na kimataifa.

Karantini inakusudiwa kutenganisha watu ambao walikuwa na mawasiliano ya karibu na mtu mwenye maambukizi ili wasiambukize watu wengine. Kwa sasaCDC haishauri kuwaweka karantini watu ambao wameathiriwa na Covid-19 lakini hawajaambukizwa. (Tazama CDC: Kuzuia Magonjwa ya Kupumua.)

Kutengwa huwatenganisha watu ambao wamethibitishwa au wanashukiwa kuwa na COVID-19 na kuwaweka mbali na wale wasiokuwa na COVID-19. CDC inapendekeza kwamba ukae nyumbani na mbali na wengine (ikiwa ni pamoja na watu unaoishi nao ambao si wagonjwa) ikiwa una dalili za virusi vya kupumua ambazo hazijaelezewa vyema na sababu nyingine. Dalili hizi zinaweza kujumuisha homabaridiuchovukikohozipua zinazotoa makamasina maumivu ya kichwakati ya dalili zingine. Kwa siku 5 baada ya dalili kuimarikaunapaswa kuchukua tahadhari zaidikama vile kuboresha uingizaji hewa kwa kufungua madirisha ili kuingiza hewa safi kutoka nje au kusafisha hewa ya ndanikunawa mikono mara kwa mara na kusafisha sehemu zinazoguswa mara kwa marakuvaa barakoa inayokuenea vizurikuweka umbali kutoka kwa wenginena kuendelea kujipima kabla ya mikusanyiko yoyote. Hii ni muhimu sana kulinda watu wenye mambo ambayo huongeza hatari ya ugonjwa mkali kutokana na virusi vya kupumua. (Tazama pia CDC: Kuzuia Kuenea kwa Virusi vya Kupumua Unapokuwa Mgonjwa.)

Taarifa Zaidi