×

注意!页面内容来自https://sw.hesperian.org/hhg/Virusi_vya_Korona,本站不储存任何内容,为了更好的阅读体验进行在线解析,若有广告出现,请及时反馈。若您觉得侵犯了您的利益,请通知我们进行删除,然后访问 原网页

Hesperian Health Guides

Virusi vya Korona — COVID-19

COVID-19

COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi (kirusi cha korona) ambacho kinaweza kuenea baina ya watu. Dalili za kawaida za COVID-19 ni kikohozi kikavuhomana maumivu ya mwili. Baadhi ya watu pia hupumua kwa shidana hupatwa na maumivu kooni. COVID-19 mara nyingi huathiri mfumo wa kupumua. Watu wengi hupona COVID-19 bila kuhitaji matibabu rasmi lakini wengine huugua sanahasa watu wenye umri mkubwa na wengine wenye matatizo ya kiafya kadhaa(angalia chini). COVID-19 inaweza kusababisha nimonia (maambukizi makali kwenye mapafu) ambayo yanaweza kuathiri mapafumoyofigona katika matukio hatari zaidi kusababisha kifo. Baadhi ambao hupona COVID-19 huendelea kupatwa na matatizo ya kiafya kwa miezi au hata miaka kadhaa(matatizo ya kiafya ya COVID ya muda mrefu au Long COVID).

Virusi hubadilika muda wote na kutengeneza aina mpya za virusi tofauti na kirusi cha awali. Aina mpya za virusi vya COVID-19 zinaendelea kuibukana baadhi ya virusi hivi huenea haraka na kwa urahisi zaidi kuliko vingine. Chanjo hukukinga usipatwe au usiambukize aina yoyote ya virusi vya COVID-19na kuna njia zingine ambazo unaweza kutumia kujikinga wewe mwenyewe na jamii yako pia.

Je virusi vya COVID-19 husambaa namna gani?

watu wawili ambao hawajavaa barakoa wameketi karibu na mwinginemoja akikohoa kwenye mkono wake

Kirusi cha COVID-19 huingia mwilini mwako kupitia mdomo wakopua na macho pale mtu aliyeambukizwa anapopumuakukohoaau kupiga chafya karibu yako. Kirusi hiki husambaa kwa urahisi zaidi katika sehemu zisizopitisha hewa vizuri na penye msongamano wa watu na ambao hawajavaa barakoa. Hivyouwezekano wa kupata COVID-19 kutoka kwa watu wengine unakuwa mkubwa zaidi unapokuwa ndani ya jengokwenye msongamanoau bila barakoa iliyofunika mdomo na pua yakoukilinganisha na unapokuwa njeunapoepuka makundi makubwa ya watuna unapovaa barakoa.

Watu wengi huanza kuugua ndani ya siku 5 baada ya kupata maambukizi lakini virusi vya COVID-19 vinaweza kuishi ndani ya mwili kwa siku 2 hadi 14 kabla ya dalili za ugonjwa kuanza kuonekana. Na baadhi ya watuhasa watotowanaweza kupata maambukizi lakini wasioneshe dalili ya ugonjwa huu. Hivyowatu wanaweza kuwa na virusi vya COVID-19 bila kujijua na wanaweza kuvisambaza kwa watu wengine.

Nani anaweza kuambukizwa virusi vya COVID-19?

Mtu yoyote anaweza kuambukizwa virusi vya COVID-19. Watu ambao wamechanjwa au waliowahi kuupata ugonjwa huu wana uwezekano mdogo wa kupatwa na COVID-19na kama wataupatakawaida unakuwa siyo mkali. Watu wenye umri zaidi ya miaka 60 na wale wanaougua magonjwa ya upumuajikisukarimatatizo ya moyo na wenye mifumo ya kinga dhaifuwana uwezekano mkubwa wa kuugua sana wanapopatwa na COVID-19.

Watu wawili waliovaa barakoa wameketi mita 2 kutoka kwa mwingine wakiongea.

Unawezaje kuzuia maambukizi?

Kupata chanjo ya kisasa zaidi ya COVID-19 kila inapopatikana chanjo mpya ndiyo njia bora zaidi ya kujikinga dhidi ya COVID-19 na magonjwa yanayoambatana kwako na wengine. Kwa sababu chanjo hizi hazipatikani katika sehemu nyingi za duniani muhimu kuchukua hatua zingine kujikinga wewe mwenyewe na jamii yako.

  • Vaa barakoa: Kuvaa barakoa hukupunguzia uwezekano wa kusambaza virusi vya COVID-19 kama tayari unavyona hukupunguzia uwezekano wa kupata virusi hivyo kutoka kwa watu wanaokuzunguka. Watu wengi katika jamii yako wanapokuwa na COVID-19na unalazimika kuwa karibu na watu wengiau kukaa ndaniuvaaji barakoa unaweza kukukinga usiambukizwe COVID-19.
  • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni au tumia kitakasa mikono chenye kemikali ya kuua vijidudu(sanitaiza) kama huna sabuni na maji. Hii ni muhimu zaidi hasa unapokuwa unarudi nyumbanibaada ya kutumia choo au kumtawaza mtotokabla ya kula na baada ya kukohoakupiga chafya au kupenga kamasi au hata kufikicha pua yako. Epuka kugusa uso wako kabla ya kunawa mikono yako.
  • Boresha mfumo wa upitishaji hewa: Kutana na wengine nje ya nyumba ili kupunguza kiasi cha virusi utakavyokumbana navyo. Kama uko ndani ya nyumba,fungua madirisha na milango ili kuruhusu hewa safi kuingia.
  • Kama mmoja wapo kwenye kaya atapata COVID-19: Mgonjwa anapaswa kubaki nyumbani na kujiweka mbali na watu wengine kwenye kayakadri itakavyowezekana. Kila mtu anapaswa kuvaa barakoa anapokuwa chumba kimoja na mgonjwa huyu.
  • Fuatilia afya yako: Kama umekuwa na mgusano au kukaribiana na mtu mwenye COVID-19 jiangalie kama una dalili zozote za ugonjwa huu. Kama una dalili za COVID-19baki nyumbanijiweke mbali na wengine na pata kipimo cha COVID-19 kama unaweza. Tumia vipimo vinavyotoa majibu haraka(rapid tests) kama unavyoau muulize mfanyakazi wa afya wapi unaweza kupata kipimo.Vaa barakoa kila unapokuwa na watu wengine.
  • COVID- 19 inatibiwaje?

    Watu wengi wanaopatwa na COVID-19 hupona nyumbani bila matibabu rasmi. Katika matukio kama hayaCOVID-19 hutibiwa kama magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi- kwa kupumzika na kunywa maji ya kutoshasupuna vinywaji vinginena kwa kutibu maumivu na homa yoyote kwa dawa ya parasetamo(acetaminophen) au ibuprofeni. Kwa sababu COVID-19 husababishwa na kirusidawa za antibiotiki hazitaweza kuponya ugonjwa huu au kusaidia watu kupata nafuu.

    Katika maeneo mengiwatu wenye virusi vya COVID-19 na ambao wanaweza kuugua vibaya sana (kwa sababu ya umri au matatizo mengine ya kiafya) wanaweza kutumia dawa za kupambana na virusi kuwasaidia kujisikia ahueni zaidi. Dawa hizi lazima zianze kutumika ndani ya siku chache za kwanza baada ya dalili za COVID-19 kuonekana. Kama una COVID-19ongea na mfanyakazi wa afya mara moja ili kujua fursa za matibabu zilizopo.

    Hatari kubwa zaidi kutokana na ugonjwa mkali wa COVID-19ni kushindwa kupumua. Matibabu kwa ajili ya matukio makali ya ugonjwa huu yatajumuisha oksijeni na kifaatiba maalum cha kumsaidia mgonjwa kupumuaambavyo hupatikana tu katika vituo vya kutolea huduma za afya.


    Ukurasa huu ulihuishwa: 02 Julai 2024